NEWS



CHADEMA WAIBOMOA NGOME YA MAGUFULI

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kagera kimeisambaratisha ngome ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, baada ya kufanikiwa kuwahamisha viongozi na wanachama 80 wa CCM akiwamo kada maarufu, Dk. Benedictor Lukanima.
Vua gamba vaa gwanda ndani ya Chato.

Viongozi na wanachama hao wa CCM wakiongozwa na Dk. Lukanima, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Norte kilichopo nchini Colombia, walitangaza rasmi kuvua gamba na kuvaa gwanda katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chato mjini, na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kagera, Alfred Mganyizi Rwagatare.
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Dk. Lukanima
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jimbo na wilaya hiyo ya Chato, Wana CCM hao waliohamia CHADEMA walikiponda vikali chama tawala, kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kuwasaidia wananchi kuondokana na kero nyingi, ukiwemo umaskini wa kupindukia unaozidi kuota mizizi hapa nchini.
Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Makonzela Phinias.
Baadhi ya viongozi wa CCM waliohamia CHADEMA ni pamoja na Makonzela Phinias ambaye alikuwa mjumbe wa UVCCM na mwakilishi wa mkutano mkuu wa Vijana Mkoa wa Geita, Masunga Maswanzali, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Nyasenga, Kijiji na Kata ya Ilemela, Josephat Manyenye ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM pamoja na Dk. Benedictor Lukanima, ambaye mwaka 2010 alishika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya chama hicho tawala.
Makusanyo ya kadi yakiendelea.
Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare alimrushia kombora zito Waziri Magufuli kwa madai kwamba, kiongozi huyo ameshindwa kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, ikiwamo ya uhaba wa huduma ya maji, afya, elimu na fursa za kiuchumi jimboni humo.
Kadi zilizorejeshwa.
Lwakatare alimuita Dk. Magufuli bingwa wa takwimu aliyeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake, licha ya kuwa waziri kwa muda mrefu serikalini. "Magufuli ni bingwa mkubwa wa takwimu. Anaweza kuwaambieni hadi samaki walio na mimba Ziwa Victoria. Lakini ameshindwa kutoa takwimu za wanafunzi wanaokwenda shuleni bila viatu wala ‘yebo yebo’.
"Wakati umefika sasa wananchi wa Chato kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za hasira baina ya CCM na huyu Magufuli, kisha kuwachagua viongozi wa CHADEMA kwa maendeleo yenu," alisema Lwakatare.
Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio nayo amani ikatawala.
 Kuhusu bei ya pamba, Lwakatare ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), kabla hajahamia CHADEMA, alisema: "Serikali ya CCM pamoja na Magufuli imeshindwa kuwasaidia wakulima wa zao hili la pamba."
Dk. Lukanima na wenzie wakitoka kwenye mkutano.
Kwa upande wake, Dk. Lukanima aliituhumu CCM na serikali kwa kukosa mwelekeo wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
"CCM imekosa mwelekeo. Mimi na usomi wangu huu siwezi kuendelea kuwa ndani ya CCM ambayo naiona haina faida kabisa kwa Watanzania wenzangu. Hivi niwaulize ni yupi mwenye unafuu aliyeshika chuma cha moto na aliyeshika ubao?

"Jibu ni aliyeshika ubao...kwa hiyo njooni tujiunge na CHADEMA kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii. Mfano, hapa Chato hakuna fursa za kiuchumi, mashirika yamekufa, huduma za kijamii mbovu, na anayeng’ang’ania CCM ni sawa na usaliti mkubwa wa maendeleo ya taifa hili," alisema Dk. Lukanima.

Aliwaomba wananchi wa Chato, mkoa na taifa kwa ujumla kukiunga mkono Chama hicho cha CHADEMA, ili kujikomboa na adha mbalimbali zinazolikabili taifa na wananchi wake, na kwamba kilichomsukuma kuhamia chama hicho cha upinzani ni kwenda kuongeza nguvu katika vuguvugu la mabadiliko.



TAARIFA IFUATAYO NIMEIPATA JAMIIFORUMS:
Kuna mbinu chafu zinapangwa katika kuficha ukweli wa kile kilichotokea kwa dr. Ulimboka. Mbinu hizi zinalenga kuficha maovu yaliyofanywa na serikali kwa dr ulimboka na hivyo kuisafisha serikali ili ionekane kuwa haihusiki na unyama huu.

Mtu aliyekuwa anajitambulsha kwa dr. Ulimboka na kuwa na mawasilinao nae kwa mda mrefu akitumia jina la Abduel (si jina lake halisi na wengine humuita abedi) alikabidhiwa kazi ya kumfatilia dr ulimboka siku mbili baada ya waziri mkuu pinda kwenda kuonana na madaktari pale Muhimbili. Kitu cha kwanza alichofanya ni kujiweka karibu na ulimboka katika kuzungumzia matatizo yao lakini pia huyu jamaa alikuwa link kati ya ulimboka na serikali. Katika kipindi chote hicho mwanausalama huyu likuwa akimfatilia ulimboka ili kumjua kwa undani zaidi.

Baada ya kuona msimamo wa dr ulimboka juu ya swala hili la madaktari hautetereki na habadiri msimamo wake maana walishataka kumpatia pesa ili anyamaze ; ndipo sasa maandalizi ya kumnyamazisha kwa kutumia formula ya ’’ maiti haisemi’’ yalianza. Lengo lilikuwa ni kumuua kabisa na hiyo juzi walidhani wamemuua.wazo la kumnyamazisha jumla ulimboka halikutoka kwa huyo mwana usalama bali nae alipokea maelezo toka juu kwa watawala. Mpango wa kutekwa ulimboka ulipangwa na kitengo anachofanyia kazi mwana usalama huyo na kutekelezwa na maafisa wapolisi waliokabidhiwa jukumu hilo.

MBINU CHAFU
Baada ya kufanikiwa kumteka na kumpiga vibaya dr ulimboka na hatimae kumtupa huko msitu wa pande huku wakidhani tayari adhma imetimia ya kumtoa uhai sasa serikali dhaifu imepanga mipango michafu ili kujisafisha ili isionekane kuwa imehusika na unyama huu.


1. Abduel amesafirishwa na kuondolewa nchini Tanzania usiku wa tarehe 27 kwa kupita Nairobi na baadae ataelekea kwenye ubalozi wa afrika ya kusini atakapopangiwa majukumu mengine. Hii yote ni katika kuficha ukweli . hao maafisa wa polisi watano waliomteka ulimboka wapo nchini na mmoja amewekwa kwenye tume ya kuchunguza utekwaji nyara wake iliyoundwa na kova nahii imefanywa makusudi kwa malengo flani; wanne waliobaki wamesambazwa kwenda mikoan na hawapo dar.


2. Kamanda wa polisi kova ameelekezwa KUHAKIKISHA anailinda serikali katika jambo hili na afanye awezalo kuonyesha umma wawatanzia kuwa serikali haihusiki na jambo hili.katika kuficha na kuilinda serikali kova, mwema na maafisa wa wajuu wa usalama wa taifa walishauliana ili kuilinda serikali na kadhia hii mahabusu 5 wenye makosa ya ujambazi wanahitajika kutoka katika magereza yaliyopo mwanza, songea, tabora, tanga na kigoma waletwe dar ili hao waweze kuonyeshwa kwenye vyombo ya habari kuwa ni majambazi yaliyomteka ulimboka na kumpiga. wakishapatikana wataonyeshwa kwenye vyombo vya habari na umma wa watanzania utaambiwa kuwa wale ndio walifanya unyama huo wako chini ya ulinzi na kuwa maohojiano yanaelendelea na uchunguzi ukikamilika watapelekwa mahakamani na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mchezo.
3. mbinu nyingine ni kuwa mahabusu hao wasafirishwe hadi pwani na wauwawe wote na taarifa itoke kuwa ndio waliomteka dr ulimboka na wamekamatwa wakiwa mkoa wa pwani katika msako mkali wa jeshi la polisi. Na katika kujibizana risasi polis ilifanikiwa kuwaua majambazi hayo. Na hapo ndo itakuwa mwisho wa swala hili na serikali itakuwa imenawa mikono na kujisafisha

Kwa sasa kinachofanyika ni kuwasiliana na magereza husika ili kila gereza litoe mtu mmoja (mahabusu) atakayesafirishwa hadi dar/pwani na wataunganishwa kisha kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari wakiwa hai au maiti ili kuuaminisha umma kuwa wao ndio walimvamia dr.ulimboka
Upelelezi na uchunguzi unaofanyika sasa ni changa la macho kwa watanznai na hiyo tume aliyoiunda kova nayo ni changa la macho ,na kamaulimboka alifanikiwa kuwaona vizuri na kuzishika sura zao ,mmoja wao yupo katika kamati hiyo. hakuna uchunguzi wowote utakaofanyika wenye tija kwa taifa juu ya kilichotokea.Kamanda Kova anasimamia operation hii na ameambiwa HAKIKISHA serikali inasafishika.

Mazingira yote yanayoihusisha serikali kwa watu wake kufanya ushenzi kuna jitihada kubwa inafanyika ili kufuta dhana hiyo. Si maraya kwanza kwa serikali kuua watu inaowaona ni mwiba kwake. Wapo wengi na wengi wamezikwa kwenye msitu huo wa pande, kuna msitu uko kibaha(kama uamzi wa kuwaua mahabusu utakubaliwa basi watauliwa kwenye msitu huo) na wengine hutupwa baharini .
Kusamilika kwa ulimboka ni kuwa Mungu ana mpango nae na serikali inafanya kila linalowezekana kujinasua. si wote serikalini wamefurahishwa na kilichotokea wengine wamechukia tena sana



BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi
madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo
ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao
waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari
18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti
kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo
la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.
"Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na
kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe
23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na
Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi
19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns
doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012
ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura
kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa
uamuzi.
Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na
madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika
na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao
waligoma.
Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali
ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za
kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka
kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

"Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha
ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma,
madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye
ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote
mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza
hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya
Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano
wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.
https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif


KUTOKA MWANZA BUGANDO  BMC
Habari za uhakika kutoka ktk hospitali ya Bugando madaktari waligomo waamriwa kufungasha mizigo yao na kutoka katika majengo ya hospitali hiyo chini ya ulinzi wa FFU.

Baadhi ya madaktari hao wa mafunzo ya vitendo wameondoka usiku huu baada ya kuogopa lakini wengine wamebakia.

Baada ya majadiliano baina ya FFU na uongozi wa BMC wameamua kuwacha waliogoma kutoka mpaka kesho kuepusha fujo ktk maeneo hayo na usiku huu,so kesho ngoma ya kuwatimua ipo pale pale....

Kwa wale ambao wana watu wanaowafaham mnaweza kuendelea kudadisi zaidi nini kinaendelea kwa wakati huu.

KUTOKA DODOMA HOSPTAL
WAKATI mgomo wa madaktari ukiendelea katika mikoa mbalimbali,
Madaktari 11  wa mafunzo kwa vitendo katika Hospital ya Mkoa wa Dodoma
wamesimamishwa kazi kutokana na kuendelea na mgomo.
https://mail.google.com/mail/images/cleardot.gif



Kujeruhiwa Kwa Dr. Ulimboka; KCMC Kugoma Rasmi

Daniel Mjema na Rehema Matowo
TUKIO la kujeruhiwa vibaya Dk Stephen Ulimboka, jana kulilichochea hasira ya madaktari ambapo kundi la madaktari liliingia wodi hadi wodi katika hospitali ya rufaa ya KCMC na kuwatoa madaktari kazini.

Taarifa zilizopatikana hospitalini hapo zilisema, madaktari hao waliwatoa kwa nguvu wenzao waliokuwa wakiendelea kutoa huduma katika hospitali hiyo wakiwamo madaktari raia wa kigeni.“Ni balaa maana madaktari wameingia wodi moja hadi nyingine hadi wodi ya wazazi na kutushurutisha tusitishe kutoa huduma kama njia ya kupinga kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka”, alidai mmoja wao.
Madaktari hao walikuwa wakitembea na Laptop zikiwa na picha za Dk Ulimboka, akivuja damu huku wengine wakiwa na picha zilizochapishwa kwenye karatasi wakionyesha kila mtu wanayekutana naye.

Madaktari hao walikusanyika katika mgahawa uliopo jirani na chumba cha kuhifadhia huku wakipaza sauti wakitaka tukio la Dk Ulimboka liweke historia nchini katika kupigania haki za madaktari.
Huku wakikataa kupigwa picha wala kunukuliwa majina yao, madaktari hao wamesema watasitisha kutoa huduma zote zikiwamo za dharura kama Serikali haitatoa kauli ya kuridhisha juu ya tukio hilo.

“Pinda (Mizengo-Waziri Mkuu) si amesema liwalo na liwe basi na sisi tunasema haturudi kazini kwa sababu usalama wetu ni mdogo na sisi tunasema liwalo na liwe”walisikika madaktari hao wakisema.

Hata hivyo madaktari katika hospitali za serikali na vituo vya Afya katika wilaya za Same, Mwanga,Rombo, Hai na Moshi waliendelea kutoa huduma kama kawaida huku wakisita kutoa maoni yao juu ya tukio hilo.

Waandishi walipotembelea wodi mbalimbali na kuzungumza na wagonjwa, walisema....




Unyama: Dr Ulimboka Atekwa, Aumizwa ( Gazeti Mwananchi)

Waandishi Wetu
NI unyama. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka ametekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.Daktari huyo ambaye amekuwa akiratibu mgomo wa madaktari unaoendelea, aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu akiwa katika hali mbaya.

Baada ya kuokotwa na wasamaria wema na kufikishwa katika Kituo cha Polisi, Dk Ulimboka aliwahishwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kwa matibabu, na ilielezwa kuwa hali yake haikuwa nzuri.

Taarifa za kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka zilisambaa kwa kasi katika vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa simu.

Kutokana na tukio hilo, wanaharakati wa haki za binadamu wameituhumu Serikali kuhusika na tukio hilo, huku Serikali ikikana tuhuma hizo, na papohapo ikiagiza Jeshi la Polisi kuwasaka waliohusika.

Akisimulia mkasa huo kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika klabu ya Leaders jijini Dar es Salaam, alikokuwa na wenzake wawili.

Alisema baada ya kukaa kwenye baa hiyo kwa muda, alianza kujisikia vibaya tofauti na siku zingine.

"Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk. Ulimboka)," alieleza na kuongeza,

"Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini ilikuwa haina namba."

Taarifa zaidi zilizolifikia Mwananchi kutoka Moi alikolazwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu, zilieleza kuwa baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa daktari huyo aliteswa vibaya, ikiwamo kuumizwa sehemu za siri, kuvunjwa meno kadhaa, mbavu na miguu.

Habari zaidi zilisema kuwa, baada ya kufikishwa katika Msitu wa Pande na kupata kipigo, alizimia kwa muda na alipozinduka aliwachomoka watekaji hao na kujaribu kukimbia.

Msitu wa Pande ulioko wilayani Kinondoni, ndiko wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam waliuawa na polisi mwaka 2006.

Chanzo chetu cha habari kilisema, baada ya Dk Ulimboka kujaribu kuwatoroka watekaji, walipiga risasi mbili hewani, aliposimama wakamshika na kumpa kipigo na mateso zaidi, hivyo kusababisha avunjike maeneo mbalimbali ya mwili.

Polisi waunda tume
Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk Ulimboka.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa tukio hilo ni la aina yake na kwamba halijawahi kutokea hapa nchini.

Alisema jopo hilo ambalo linaongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi linahusisha wapelelezi wa fani mbalimbali.
“Ni issue (jambo) ambayo imetokea bila kutegemea katika namna ambayo ina utata, hivyo kazi yetu ni kutegua utata huo,” alisema Kova na kuongeza:
“Hatutaki katika nchi yetu matukio kama haya yawe ya kawaida, tunataka liwe la mwanzo na la mwisho.”

Kamanda huyo alisema yeye alipata taarifa za kutekwa Dk Ulimboka usiku wa kuamkia jana saa 7 usiku.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, Dk Ulimboka aliokotwa na raia mwema katika eneo la Msitu wa Pande jana saa 2:30 asubuhi karibu na barabara huku akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili, ikiwamo kichwani na mikononi.
Alisema raia huyo (jina limehifadhiwa) alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Bunju, na askari walikwenda kwenye gari la raia huyo na kumkuta Dk Ulimboka wakamchukua na kwenda naye ndani.
 Kova alisema: “Aliyemuokota alisema alimkuta amefungwa mikono na miguu, na inaonekana kama watu hao walikuwa wanalipiza kisasi.”
Kwa mujibu wa kamanda huyo, akiwa kituoni hapo, Dk Ulimboka alijieleza kwamba juzi saa 5:30 usiku akiwa katika klabu ya Leaders na wenzake wanapata vinywaji pamoja na wateja wengine, walikuja watu watano na kuwatishia.
Alisema watu hao waliwataka walale chini na kwamba walitii, kisha watu hao walimchukua Ulimboka na kuwaambia wengine waendelee na vinywaji.
“Ulimboka alisema watu hao walikuwa na gari aina ya Escudo lenye rangi nyeusi na hili gari halikuwa na namba na walichukua ufunguo wake wa gari, nyaraka kadhaa na hela alizokuwa nazo,” alisema Kova.
Alisema akiwa katika gari hilo na watu wengine watano, ghafla walianza kumpiga huku wakiwa hawasemi chochote na kwamba baadaye walimfunika kichwani na fulana nyeusi hadi Msitu wa Pande.
Kova alisema baada ya maelezo hayo, Dk Ulimboka alitoa namba za simu za rafiki yake Dk Deogratius, na baada ya hapo alipewa fomu ya matibabu (PF3) na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu.
Kamanda huyo alitoa wito kwa wananchi na mtu yeyote mwenye taarifa kamili kuhusu tukio hilo atoe taarifa, kwani lisipojulikana vizuri linaweza kuzua minong’ono mingi.
Askari ajeruhiwa MNH
Katika hatua nyingine, Kova alisema watu wasiojulikana wamemjeruhi Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi cha Selander Bridge ambaye alikwenda MNH kufanya upelelezi wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kova, Mkuu huyo wa upelelezi alijeruhiwa wakati akiwa anaongea na simu, na kwamba watu hao pia walimpora vitu alivyokuwa navyo ikiwemo simu.
Mkurugenzi Moi

Mkurugenzi wa Tiba katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), Cuthbert Mchalo alisema majeruhi huyo alifikishwa hospitalini hapo saa 4:25  asubuhi, kwa msaada wa gari la wagonjwa la Kampuni AAR, kutoka Kituo Kidogo cha Polisi Bunju.

“Tumempokea, anaendelea vizuri na amepata maumivu katika maeneo ya kifuani, kichwani na tumboni,” alisema na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Alifafanua kwamba kwa sasa wanajitahidi kumpatia matibabu, ingawa alipelekwa hospitalini hapo akiwa katika hali ambayo siyo nzuri, na uchunguzi zaidi unaendelea.

Wanaharakati walaumu Serikali
Miongoni mwa watu wa kwanza kufika katika Kituo cha Polisi Bunju kumuona Dk Ulimboka ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba ambaye alisema kilichotokea kinaonyesha jinsi gani Serikali ilivyo na woga katika kushughulikia  matatizo ya wananchi.

Dk Bisimba alisema wao wanaamini kuwa tukio hilo lina mkono wa Serikali na kama ni kinyume cha hapo, basi inapaswa kuwaridhisha wananchi kuwa hawana mkono wao katika sakata hilo.

“Kama wao hawana mkono wao basi wanapaswa kuwaridhisha wananchi kuwa hawahusiki kwa kuwatia mbaroni wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria,” alisema Bisimba.

Mkurugenzi huyo alisema matamshi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bungeni jana kuwa wanashughulikia suala la madaktari na watalimaliza liwalo na liwe inaleta tafsiri kuwa kilichotokea kina mkono wao.

“Alivyosema liwalo na liwe na kinachotokea sasa kinabainisha kuwa mengi zaidi yatafuata,” alisema Bisimba na kuongeza kuwa hali hiyo inasikitisha na haikuwahi kufikiriwa.

Bisimba alisema baada ya wasamaria kumkuta mnamo saa 12:00 asubuhi, walimpeleka katika kituo kidogo cha Polisi cha Bunju ambako polisi walifungua mashtaka ya wizi wa maungoni na kupatiwa RB yenye namba BJ/RB/1870/2012.
“Mimi nilipata taarifa za kutekwa kwake kutoka kwa mwenzie aliyekuwa naye mnamo saa nane usiku, na baada ya kupata taarifa hizo niliwaeleza wanaharakati wenzangu juu ya hatua za kuchukua,” alisema Bisimba.

Bisimba alisema aliwasili katika Kituo cha Polisi cha Bunju, jana mapema asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya, lakini hakuwa amepatiwa huduma yoyote.

“Tulikwenda kumchukua na kukuta hali yake ni mbaya, lakini cha ajabu pamoja na majeraha yote hakupatiwa msaada wowote wa huduma, jambo ambalo lilitusikitisha sana,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sikika, Irenea Kiria alisema kilichotokea ni kitu kibaya na kinaonyesha jinsi gani Serikali inavyoshughulika na watu, badala ya kujali hoja za msingi ambazo zinawasilishwa.

Kiria alisema hoja za madaktari zilipaswa kusikilizwa kwani licha ya madai ya masilahi yao lakini pia wanapigania mazingira bora yenye utu kwa ajili ya wagonjwa.

Madai mengine ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wananchi pamoja na upatikanaji wa dawa, mambo ambayo alisema hayahitaji mjadala.

“Suala la masilahi ya madaktari linazungumzika lakini siyo suala la dawa, mazingira bora ya kuwahudumia wagonjwa na upatikanaji wa vifaa tiba na vipimo vingine,” alisema Kiria.

Nchimbi: Tutawasaka
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi alisema Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika na utekaji huo.

Dk Nchimbi alisema mjini Dodoma kuwa Serikali haihusiki kwa namna yoyote ile na utekaji nyara huo, na kwamba kitendo hicho kinapaswa kulaaniwa kwani hakikubaliki katika jamii hasa kwa zama hizi.

“Kwanza, madaktari ni watu muhimu ambao wao ndio wanaotuwezesha sisi kuishi, kwa hiyo wapo kwa ajili ya maisha yetu, hata kama asingekuwa daktari, kwa mtu yeyote yule, jambo hili halikubaliki katika nchi yetu,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza:

“Tumewaagiza polisi wafanye uchunguzi ili kuwabaini wahusika na wakipatikana wafikishwe katika vyombo vya sheria, maana hatuwezi kwa namna yoyote kuvumilia vitendo vya aina hii.”

Alisema Serikali imestushwa sana na tukio hilo na haitavumilia kwa namna yoyote vitendo hivyo pamoja na vile vya unyanyasaji kwani ni kinyume cha sheria.

Kuhusu kupigwa kwa Mkuu wa Upelelezi (OC- CID), ASP Mukiri, Dk Nchimbi alisema lilikuwa ni tukio la bahati mbaya kwamba madaktari waliokuwapo Muhimbili walishindwa kuwa na uvumilivu kwani askari aliyepigwa alikuwa ameagizwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela kwenda kufuatilia matibabu ya Dk Ulimboka.

“Hapa ndipo ninapotofautiana na watu wengi, mnampigaje polisi, maana yule anapaswa kuwa rafiki wa raia, sasa unampigaje mtu ambaye ni mlinzi na umemwajiri, analipwa kwa kodi yako?” alihoji Dk Nchimbi.

Yaliyojiri bungeni
Tukio hilo lililosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, liliibuka bungeni, ambako Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alilaani vikali kitendo cha watu wanaodaiwa ni maofisa wa vyombo vya usalama kumpiga Dk Ulimboka.Alisema kitendo hicho ni unyama unaostahili kukemewa na kila mpenda amani hapa nchini.

“Tumestushwa na tukio hilo na tunalaani vikali kitendo hicho na kumwombea Dk Ulimboka ili apone haraka,” alisema Mdee.Katika hatua nyingine, Mwananchi lilitembelea hospitali za Mwananyamala, Temeke na Amana, kujionea hali ilivyokuwa baada ya kusambaa kwa taarifa za kupigwa kwa Dk Ulimboka.
Katika hospitali ya Mwananyamala, wengi walioonekana walikuwa ni wauguzi huku madaktari wakidaiwa kwenda katika hospitali ya Muhimbili kumuona mwenzao aliyejeruhiwa.
Dk Ulimboka aliwahi kufanya kazi katika hospitali hiyo ya Mwananyamala katika miaka ya nyuma.

Hata hivyo, juhudi za waandishi kuzungumza na uongozi wa hospitali hiyo, hazikufanikiwa baada ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mganga Mkuu kusema kuwa mganga huyo amekataa kuzungumza, akiwataka waandishi wafike ofisini kwake leo.
“Ameniambia niwapeleke kwa katibu wake, lakini na yeye nimemkosa, sasa nimerudi kwake ameniambia niwaambie mrudi kesho,” alisema katibu muhtasi wake.
Katika hospitali za Temeke na Amana, hali pia ilikuwa hivyo, baadhi ya wahudumu waliokutwa katika hospitali hizo wakikataa kuzungumza kwa madai kuwa wanaotakiwa kuzungumza hawapo.

Madaktari jeshini waitwa kazini
Taarifa zilizotufikia wakati tukienda mitamboni, ambazo hazijathibitishwa, zilieleza kwamba madaktari wote wanaofanya kazi kwenye hospitali za jeshi ikiwamo Lugalo ambao hawakuwa zamu jana jioni, waliitwa kazini, tukio ambalo linahusishwa na tamko la Serikali linalotarajiwa kutolewa leo.

Imeandikwa na Nora Damian, Boniface Meena,  Fredy Azzah, Elizabeth Edward, Geofrey Nyang’oro, Zakhia Abdallah , Joseph Zablon, Raymond Kaminyoge, Aidan Mhando, Dar; Neville Meena, Dodoma

***********************************************

Mgogoro Wa Madaktari Na Serikali Ni Balaa Kwa Taifa

Ndugu zangu,

Nimepitia nilichoandika Februari 4, 2012 juu ya mgogoro wa madaktari na Serikali nikaona ni vema niyarushe tena maandiko yangu yale kama yalivyokuwa, bila kuongeza au kupunguza neno. Maana, kuna ambacho wahusika wanaweza hawakukiona wakati ule, lakini wakakiona sasa. Soma nilichoandika...


Ndugu zangu,


Mgomo wa madaktari wetu ni habari kubwa. Umeingia sasa kwenye wiki ya pili. Hata kama ungekuwa ni wa siku mbili, bado ungesababisha madhara makubwa kwa nchi. Kwamba sasa una zaidi ya siku kumi na nne ni balaa kubwa kwa nchi yetu.


Tafsiri yangu;


Uliopo ni mgogoro kati ya madaktari na Serikali. Na kwenye mgogoro kama huu, siku zote, wenye kuathirika zaidi ni wananchi walio wengi.


Ni ukweli, kuwa karibu kila Mtanzania anayeamka asubuhi, ama ni mgonjwa au ana ndugu, jamaa au rafiki aliye mgonjwa.


Hivyo basi, kuna mamilioni ya Watanzania wenye kutaabika kila siku na maradhi ya aina mbali mbali. Ni Watanzania wenye kutegemea sana huduma ya tiba inayotolewa na madaktari wetu. Na katika nchizetu hizi, daktari ni rafiki muhimu sana wa mwananchi.


Ni jambo baya sana, pale Serikali inapoingia kwenye mgogoro na madaktari. Inapoingia kwenye mgogoro na marafiki wa wananchi. Hakuna mahali popote duniani wananchiwakatokea kuwachukia madaktari.


Hivyo basi, ni balaa pia pale Serikali inaposhindwa kumaliza tofauti zake na madaktari wa wananchi kwa njia ya mazungumzo na hata kufikia hatua ya madaktari kugoma.


Katika nchi zetu hizi, mganga wa tiba aliyesomeshwa kwa fedha za walipa kodi na kwa miaka mingi anahitajika sana. Mganga wa tiba msaidizi anahitajika sana. Na hata kama angelikuwapo Msaidizi wa Mganga Msaidizi wa tiba , naye angehitajika sana. Vivyo hivyo kwa wakunga wakuu na wasaidizi, wauguzi wakuu na wasaidizi wao. Wote hao anahitajika sana.


Na katika nchi zetu hizi, Serikali hazipaswi kufikia hatua ya kuwatisha na hata kuwafukuza kazi madaktari. Hilo la mwisho lifanyike tu pale ambapo njia nyingine zote za kumaliza tofauti na kusuluhisha migogoro na madaktari zitakapokuwa zimeshindikana. Na kwanini ishindakane?


Tufanye nini sasa?

Taarifa kwamba Kamati ya kudumu ya Bunge inayohusika na masuala ya huduma za jamii imepanga kukutana na madaktari wetu ni hatua njema na ya busara. Maana, katika mgogoro huu taarifa zimekuwa zaidi za upande mmoja; upande wa Serikali. Ni wakati sasa pande zote mbili zikasikilizwa na Kamati hiyo ya Bunge. Ndio, ni wakati pia hata madaktari wetu wakapewa nafasi tuwasikie.


Huu si wakati wa kufanya "propaganda" za kisiasa kwenye masuala ya afya za wananchi. Na hata pale Waziri wa Afya alipokaririwa jana Bungeni akitamka kuwa hali ya huduma za mahospitalini zimerejea katika hali yake ya kawaida ni mfano wa ’ Propaganda’ za kisiasa ambazo Watanzania hatuzihitaji kwa sasa.


Hivi ni hali gani hiyo iliyorejea kwenye kawaida yake kwenye hospitali zetu baada ya mgomo huu wa madaktari unaoendelea sasa? Kwamba askari wetu wa Jeshi la Wananchi wamelazimika kwenda kutibu wagonjwa Muhimbili hiyo haiwezi kuwa ni ’ Hali ya kawaida’. Kwamba madaktari wameripoti lakini hawaonekani mawodini hiyo haiwezi kuwa ’ hali ya kawaida’. Na kama ni kawaida, hivi ni nini tafsiri ya ’ kawaida’?


Hapa kuna ukweli unaopaswa kusemwa, na si kitu kingine bali ni ukweli. Watanzania tunataka kujua; ni kwanini watendaji wa Wizara husika wameshindwa kulitatua suala la madaktari wetu na hata kutufikisha hapa tulipo?


Yumkini, kulikuwa na hali ya kuyapuuzia madai ya madaktari katika hatua za awali. Yawezekana pia watendaji wa Wizara hawakuwa karibu na wawakilishi wa madaktari hao ili kutoa fursa ya kuongea na kutafuta ufumbuzi wa tatizo. Labda ndio maana tumefika mahali sasa mgogoro umekomaa na wahusika kuonyesha hali ya kutunishiana misuli.


Kuna mahali kosa limefanyika. Ni wapi?


Ndio hapa, kuwa hata kama Kamati ya Bunge itafaulu kusuluhisha mgogoro huu, bado Watanzania tutahitaji iundwe Tume huru itakayochunguza namna watendaji wa wizara husika walivyolishughulikia suala hili kwa upande wao.


Tume hiyo itusaidie kuupata ukweli mzima ili kama taifa, tujifunze. Na wakati tume kama hiyo itakapokuwa ikifanya kazi yake, itakuwa ni busara, kwa watendaji wakuu wa wizara husika wajiweke pembeni kwa maana ya kujiuzulu ili kupisha uchunguzi huo.


Kama Tume itabaini kuwa hakukuwa na mapungufu makubwa katika utendaji wao na hususan walivyolishughulikia suala

hili la mgogoro na madaktari, basi, itajulikana hivyo, na wana nafasi ya kurudi tena kwenye nafasi za utendaji Serikalini. Inahusu umma kurudisha imani yake kwa Serikali yao. Ndio maana ya umuhimu wa wahusika kupisha pembeni kuruhusu uchunguzi ufanyike. Maana, haitakuwa busara kuliacha suala hili likapita kama yanavyopita mengine ilihali limegharimu maisha ya Watanzania.

Na kubwa zaidi kwa sasa, ni kwa pande zote katika mgogoro huu kutambua; kuwa kwa sasa mvutano unaoendelea hautatoa mshindi, ni kwa vile, katika kilichotokea na kinachoendelea kufanyika sasa, sote, kama taifa, tumeshindwa.


Huu ni wakati wa kutanguliza busara na hekima. Tufanye yote, lakini, njia mujarab ya kutanzua mgogoro huu uliopo sasa ni mazungumzo katika mazingira ya kuheshimiana, basi.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.


Mchuma S.M








Chato Youth Movement For Democracy

We are a national movement, active at the local, regional and national level, dedicated to serving the Chato community especially the Youth. The movement is composed of Youth's and others, who share our views from the different diverse communities of Tanzania. We are all strongly united in our course, united by our common vision of purpose, bonded by the same problems we all encounter in our daily lives. We are defined as we persist, proud to operate by consensus and confident in the virtue of our goals.

Our movement is designed and devoted to increasing the awareness of and responsibility towards the political happenings in our communities, country and in the world in which we live. We call upon the youth across the country to make political engagement an important part of their lives. We urge a nation-wide focus on the current state of politics and government - and the differences each of us can make when involved in our political process.

Youth voter turnout was extremely strong in the 2010 elections. We as the Youth constitute 70% of the registered voters in our country. We must build on our momentum and strength and continue to sustain, agitate and demand Youth interests in politics and government. A lot of people are working very hard on this project. Involvement is key and crucial. Networking others is stressed, so that nobody especially the youth misses out on a movement that has the power to affect, determine and change the future of our beloved motherland. We must all harness our power and collectively bargain for our rightful shares in the leadership of this country. We must be heard!

As Youth's of this country, but particularly at CHATO we all have our diverse dreams. But all the same, dreams that are good for our country and the future generations and the entire mankind. Whether you are a primary, secondary, college, university or a non-schooling youth, we urge you to somehow be involved in public service the rest of your life. Let's join hands and make an "
Unbowed" team. The best way to accomplish something is to get involved.

Together We can Make A Difference. Pamoja Tutashinda.