Vurugu Za Zanzibar; Taarifa Za Hivi Karibuni...
Jeshi la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia Mabomu ya Machozi ili kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha Uamsho waliokuwa wamekusanyika kufanya Dua ya kuwaombea watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv. Skagit katika Mitaa ya Mbuyuni.
Habari kutoka Zanzibar zinadai kuwa Jeshi hilo la Polisi lililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kutokana na kikundi hicho cha Uamsho kuanza kuhubiri siasa badala ya kufanya Dua hatua iliyosabaisha kuvunjika kwa amani katika mitaa hiyo.
Mwandishi wa Kituo hiki cha Uhuru FM aliyeko Mjini Zanzibar amesema licha ya Watanzania kuendelea kuomboleza vifo vya watu waliokufa katika ajali hiyo, bado kikundi hicho cha Uamusho kimeendelea kufanya sisasa badala ya kufanya Dua.
Pia imeelezwa kuwa chanzo cha Mabomu hayo ya Machozi ni kikundi hicho kufanya Dua yenye utata huku masuala ya siasa yakijitokeza hatua iliyopelekea kuwepo kwa vurugu za hapa na pale hivyo Jeshi likaamua kutumia nguvu ya ziada ili kuwatawanya.
CHANZO: Radio Uhuru FM
Yanga Yaibamiza APR Mabao 2-0 Kombe La Kagame
Mchezaji
wa timu ya APR ya Rwanda, Selemani Ndikumana akijiandaa kupiga mpira
mbele ya beki wa timu ya Yanga, Kevin Yondan wakati wa mchezo wa kuwania
kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo
huo Yanga wameitwanga APR mabao 2-0 yaliyofungwa na Said Bahanuz.
Kikosi cha timu ya APR kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Chanzo: www.fullshangweblog.com
WATEJA WA VODACOM WANUFAIKA NA OFA YA MWISHO WA WIKI
- Manufaa ni kuhusu kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi, na huduma ya hifadhi habari kwa Shs, 250/- tu
- Manufaa ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi.
Wateja
wa Vodacom Tanzania wana sababu ya kufurahi kipindi cha mwisho wa wiki
kufuatia kuanzishwa kwa huduma mpya ambayo itawaruhusu kupiga simu na
kutuma ujumbe mfupi kwa gharama ya Shs. 250/- tu.
Huduma hii ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi kwenda mitandao yote.
Huduma hii ni kwa mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa saa 5 usiku hadi Jumatatu saa 1 asubuhi kwenda mitandao yote.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza huduma hii
imekuja kufuatia kubaini kwamba watumiaji wa mtandao huu huhitaji
huduma hizi kwa masaa mengi zaidi na wakati mwingine mpaka usiku mwingi.
“Tumekuja na huduma hii ili tuweze kuhakikisha kuwa tunawaridhisha wateja wetu na papo hapo wafurahi na wale wawapendao,” alisema Meza.
“Tumekuja na huduma hii ili tuweze kuhakikisha kuwa tunawaridhisha wateja wetu na papo hapo wafurahi na wale wawapendao,” alisema Meza.
Mkurugenzi
mtendaji huyo aliongeza kuwa Mtandao wa Vodacom Tanzania unaona faraja
kwa wateja na hivyo kuwa na hali ya kuwapa upendeleo mahsusi wateja
wake ili kuongeza idadi ya watumiaji.
Huduma hii inakuja wiki moja baada ya kampuni hii kuzindua huduma nyingine inayowalenga vijana wa Kitanzania ambayo inatilia mkazo wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
“Wateja wetu tayari wananufaika na matumizi ya bure ya mtandao wa kijamii wa facebook, twitter na wikepedia kupitia huduma ya “phoneson kwa wajanja”. Pia tumeingia ubia na kampuni ya Nokia ili kuwawezesha vijana kupata huduma rahisi ya mtandao yaani Internet sambamba na mauzo ya bei ya chini ya simu aina ya ZTE ambazo zinauzwa hadi Shilingi 13,000/- yote hii ikiwa ni kutaka kuwapa raha wateja wetu,” alimalizia Bwana Meza
Huduma hii inakuja wiki moja baada ya kampuni hii kuzindua huduma nyingine inayowalenga vijana wa Kitanzania ambayo inatilia mkazo wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
“Wateja wetu tayari wananufaika na matumizi ya bure ya mtandao wa kijamii wa facebook, twitter na wikepedia kupitia huduma ya “phoneson kwa wajanja”. Pia tumeingia ubia na kampuni ya Nokia ili kuwawezesha vijana kupata huduma rahisi ya mtandao yaani Internet sambamba na mauzo ya bei ya chini ya simu aina ya ZTE ambazo zinauzwa hadi Shilingi 13,000/- yote hii ikiwa ni kutaka kuwapa raha wateja wetu,” alimalizia Bwana Meza
Nimetua Stockholm, Leo Futari Tunakula Wapi?
Ndugu zangu,
Nimeingia Stockholm mchana huu. Nitakuwa hapa kwa siku tatu. Naama, Sthlm jua ni kali, na nanihii pia. Leo futari tunakula wapi? Nimekuja na samaki wa maana kwa daku. Naam, miye napenda kuvua samaki. Huko nilikotoka ukweni nimeshinda siku mbili nikivua samaki. Na mwanadamu unapovua samaki unatulia kimyaa, unatafakari pia.
Ramadhan Kareem!
Maggid Mjengwa,
0736 966032
Jenerali Ulimwengu: Nakisi Ya Usaili, Mtaji Wa Ushirikina
Hali
hii ya kutokuthamini urithi wetu imetufanya sasa tutafute walezi
wengine badala ya baba yetu, na walezi hawa ( ambao kwa hakika
hawawezi kuwa na uchungu nasi) wanatuona kama “mazuzu” wa kutumiwa na
watu wenye akili.
Wanatuona
kama punguani kwa jinsi tunavyoweza kuendelea kuwa “omba-omba” miaka
50 baada ya Uhuru wakati tunazo rasilimali ambazo wao wanazimezea
mate.
Nimewasikia,
kwa mshangao mkubwa, watawala wetu wakitamka kwamba hawajui ni kwa
nini nchi yetu ni masikini baada ya miaka yote hii na ikiwa na
rasilimali zote hizi. Huko kutotambua ndiyo sababu mojawapo kubwa ya
hali tuliyo nayo.
Haiyumkiniki
kwamba mtu anaweza kugombea uongozi wa nchi au jamii, tena kwa juhudi
kubwa na kwa kuahidi mambo lukuki, halafu baada ya kuwa ameingia
madarakani akatangaza kwamba wakati wote huo alikuwa hajui matatizo ya
jamii yake. Nini kilimsukuma kugombea?
Pasipo
na shaka akilini mwangu, sababu moja kubwa iliyotufanya tukwame kiasi
hiki imekuwa ni upuuzi wa uongozi na udhaifu wa watawala,
vikiambatana na uwezo na utashi mdogo mno wa raia kuwasaili viongozi
watawala wao na kusaili kila kilichowazunguka.
Tumefanikiwa
kujenga jamii ya watu wasio na uwezo wa kusaili mambo ya msingi
kabisa, na wasiotaka kuwasaili wale waliowakabidhi hatamu za uongozi,
hata pale hao waliokabidhiwa hatamu hizo ni dhahiri kwamba wanazitumia
vibaya; na matokeo yake ni kwamba wanawaumiza hao hao waliowaweka
madarakani, na hao wanaoumizwa hawana la kufanya.
Kukosekana
kwa utamaduni wa kusaili mambo yanayotuzunguka ndiko kunatufanya
tuendelee kuamini kwamba binadamu anaweza kupaa kwa ungo; mwili wa
albino una nguvu za miujiza; mtu anaweza kugeuka fisi na fisi akageuka
mtu; kumbaka mtoto mchanga kunatibu Ukimwi…na ujinga mwingine wa aina
hiyo.
Jamii
isiyosaili mambo ni jamii ya wajinga, na wajinga wakisha kuwa wengi
ndani ya jamii, hata weledi wachache ndani ya jamii hiyo hawafui dafu:
watanyongwa.
Ndiyo
maana tunapiga kelele siku zote kuhusu elimu bora, na elimu bora si
ile ya kumeza “maarifa” bali ni ile inayomwezesha mtu kusaili mambo
yanayomzunguka, kuuliza maswali ili apate majibu na kuuliza maswali
kuhusu majibu anayopewa, na siku zote kuendelea kusaili hata yale
mambo aliyodhani kwamba aliyaelewa awali. Ndivyo wenzetu
walivyoendelea, na ndiyo sababu wako waliko nasi tunaendelea kurejea
tulikotoka.
Bila
shaka tunahitaji kuondokana na upuuzi na ujinga tulimozama iwapo
tunataka kupiga hatua za kwenda mbele badala ya hizi za kurudi nyuma
tunazozipiga kwa kasi leo hii (kwa sababu ni kweli tunarudi nyuma kwa
kasi).
Mahali
pa kuanzia ni mwanzo, na mwanzo daima ni uongozi wa kisiasa. Siasa
safi zitazaa mazingira safi ya watu kufanya kazi za kuleta maendeleo
katika nyanja zote. Siasa hovyo zitajenga mazingira hovyo vivyo hivyo,
ambayo yataendelea kutuzamisha katika upuuzi na ujuha.
Siasa
zetu hazina budi kuwa na misingi ya usaili wa masuala yote
yanayotuzunguka, na ziachane na unafiki wa wale wanaodhani kwamba
kutosaili jambo au mtu ndio uaminifu na nidhamu.
Tukumbuke,
wale wanaodhani viungo vya mwili wa albino vinaleta utajiri, au
kwamba ungo ni helikopta, msingi wao mkuu ni kushindwa kusaili mambo
na watu.
Katika
siasa kushindwa kuwasaili wale waliokabidhiwa madaraka ya kuendesha
jamii, au kushindwa kusaili miundo, mifumo na michakato inayoendesha
jamii, ni ushirikina mwingine ambao matokeo yake ni kuidumaza jamii
yetu. Htuna budi kupambana na dalili zo zote zinazotusukuma kutokomoea
zaidi katika nakisi ya usaili.
Ndiyo
maana napingana moja kwa moja na baadhi ya mambo yanayotamkwa na
kufanywa na baadhi ya wakuu wa asasi za utawala nchini, ikiwa ni
pamoja na wakuu wa shughuli za Bunge.
Ni
kama vile wakuu hawa wa Bunge, pamoja na Spika na wasaidizi wake,
wamo bungeni kuhakikisha watawala hawasailiwi, hawadadisiwi na
hawakosolewi. Niliangalia kwa mshangao mkubwa ubishi kati ya
Spika
na mbunge aliyesema kwamba, pamoja na uzembe na upuuzi wa asasi
nyingine, alibaini pia “udhaifu wa Rais,” na hili likawa ni tatizo
kubwa lililositisha shughuli za Bunge kwa muda na likawa ni chanzo cha
gumzo nchini.
Mimi
najiuliza, iwapo mbunge wa upinzani atazuiwa kusema kwamba Rais,
ambaye ni kiongozi wa chama tawala (ndiyo kusema chama anachokipinga
mbunge huyo) ni dhaifu sasa aseme nini? Amsifu Rais kwa umahiri,
ukakamavu na ushujaa? Apendekeze kwamba Rais abakie madarakani maisha,
na chama chake kisipingwe? Kazi ya mbunge wa upinzani ni nini hasa?
Nadhani
ni kutokana na ukali wa Spika kuhusu “udhaifu” wa Rais ndiyo ofisa
mwandamizi serikalini akasimama bungeni kwa ukali kumshambulia mbunge
aliyesema kwamba baadhi ya majaji hawafai na kwamba uteuzi wao ulikuwa
wa kutiliwa shaka.
Maombolezo
Mjengwa
Blog Imeguswa na msiba huu mkubwa kwa taifa letu sisi kama sehemu ya
jamii nasi tunaomboleza siku 3 za maombolezo pamoja na watanzania wote
kwa ujumla,hivyo tunaiweka blog yetu katika rangi yeusi kwa siku 3
ikiwa ishara ya kuomboleza msiba huu wa ndugu zetu
Kikosi kazi Mjengwa Blog
Twisheni...!
Na: Elvan Limwagu wa www.limwagu.blogspot.com
Kutokana
na tukio la vifo vya watu waliokunywa Pombe kali ya Gongo hivi
karibuni, mimi binafsi napenda kuwaletea picha chache tu kuonyesha namna
pombe hiyo inavyoandaliwa.
Kule
kwetu Pombe hii huitwa kwa jina la NIPA wengine kwa kuipendezesha
wakalirefusha jina hilo kuwa "New Internationa Pure Alcohol" na kwa
hakika viongozi wengi waliotokana na makabila ya Wayao na Wamakuwa
walisoma kutokana na ADA ya mapato ya pombe hiyo kali.
Itakumbukwa
kuwa kwa mara ya kwanza katika kampeni za uchaguzi za mwaka 1995
Mgombea moja alidiriki kuwaahidi wananchi wa makabila hayo kuwa
wakimchagua ataruhusu pombe hiyo na kuiwezesha iwe inaandaliwa
kitaalamu, ingawa kura hazikutosha.
Pombe
ya Gongo au Nipa kule kwetu hutokana na Mabibo (tunda la mkorosho)
ambalo hukaushwa juani na hatimaye kuweza kuhifadhiwa hata kwa zaidi ya
miezi sita. Mabibo unayoyasikia yakishakauka hubadilika jina na kuitwa
KOCHOKO ambazo inapofika wakati wake (ni baada ya msimu wa mauzo ya
korosho kupita) hupatikana kwa adimu sana na waandaaji wake huitafuta
hata kwa maili zaidi ya 60.
Kochoko
hizo baada ya kuchambuliwa na kuondoa takataka hulowekwa kwa wiki nzima
ndani ya pipa au mtungi (chungu kikubwa) na maji yake yakipata ladha ya
juisi inayoweza kulevya (staili ya mnazi au ulanzi), ndipo huwa tayari
kwa kupikwa kama unavyoona hizo picha.
Vifaa
vilivyosababisha jungu hilo ni: Mtungi, mtutu uliounganishwa na
ngalawa, chungu kidogo cha kufunika mtungi kwa ajili ya kuzua mvuke
usitoke nje, udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kusiliba maunganisho ya
mtungi na chungu na tundu la mtutu kutolea mvuke hadi kwenye chupa.
Mvuke
unaotoka hupozwa ndani ya mtutu kwa maji baridi na kuwa maji yanayoitwa
NIPA (Gongo). Ile Pure huitwa IPACHO ambayo ni Spiriti kabisa kwa kuwa
inawaka wanapoijaribia wenyewe, ile ya mwisho inaitwa ALEKA ambayo kwa
wanaojifunza huweza kuitumia. Ili kupunguza makali ya IPACHO huwa
inachanganywa na ALEKA, hata hapo Konyagi ni cha mtoto.
Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji
MBUNGE
wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa
Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa
wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata
ya Ndago, Yohana Mpinga (30).
Jeshi
la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji
Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji
lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka
huu, majira ya jioni.
Mahojiano
hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku,
yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka
jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.
Habari
zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi
lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye
kesi hiyo ya mauaji.
Tayari
watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa
tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.
Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mauaji
hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni
huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba
magharibi.
Mauaji
hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea
kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.
Katika
hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika,
alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz
SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA UJERUMANI
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)
UMOJA WA WATANZANIA NCHINI UJERUMANI UMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA ZA AJALI MBAYA AMBAYO IMESABABISHA VIFO.
UMOJA WA WATANZANIA UNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE NCHINI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MAOMBOLEZO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU UBALIKI UMOJA WA KITAIFA
MFUNDO PETER MFUNDO
MWENYEKITI WA
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)
MFUNDO PETER MFUNDO
MWENYEKITI WA
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)
Email: kamati.utu@googlemail.com
MJENGWABLOG INATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
KWA mara nyingine, Watanzania tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea jirani na kisiwa cha Chumbe, Unguja. Ndugu zetu wapatao 60 tayari wameripotiwa kupoteza uhai. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa letu.
Mjengwablog, kama chombo cha jamii cha habari na mawasiliano kinatoa salamu za rambirambi
kwa wahanga wote wa msiba huu mkubwa. Na tunachukua fursa hii kumpa
mkono wa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete, vivyo hivyo, mkono wetu wa pole umfikie
Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Ya
Zanzibar.
Mjengwablog inaungana na Watanzania wote katika siku hizi tatu za maombelezo kwa kutorusha habari na picha za matukio yenye kuashiria sherehe na burudani.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Maggid Mjengwa
Mtendaji Mkuu, Mjengwablog.com

Ajali Ya Meli Zanzibar; Taarifa Za Hivi Karibuni....
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223 7313
Maelezo
Fax: 0255 24 2237314
E-mail:habarimaelezo@yahoo.co.uk, maelezozanzibar@zanlink.com
maelezozanzibar@hotmail.com, maelezozanzibar@gmail.com
TAARIFA YA SMZ KUHUSU AJALI YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOLEWA
USIKU HUU JULAI 19,2012
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa taarifa usiku huu ikieleza idadi ya watu waliopatikana
wakiwa hai ni 146 na kupata maiti 62.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari usiku leo,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Ali Juma Shamuhuna alisema taarifa hiyo ndio sahihi na kuwataka wananchi kutoamini taarifa
zinazotolewa na watu wengine zaidi ya Serikali.
Waziri Shamuhuna alisema kwamba maiti 62 walipatikana ambao kati ya maiti hizo watoto ni
9 na kuna raia mmoja wa kike wa kigeni ambaye hakuweza kutambulika Uraia wake,lakini
umeonekana picha yake moja ndogo ya hati ya kusafiria.
Waziri Shamuhuna alisema meli hiyo ilibeba jumla ya abiria 290 kati ya hao watu wazima 250,
watoto wadogo 31 na mabaharia 9.
Waziri huyo aliwataka wananchi katika sehemu mbalimbali hasa katika vijiji vilivyo
kandokando ya bahari watakapoona maiti au mtu akiwa hai ambaye wanadhani ni wa ajali ya
Meli ya Skagit.
Aidha, Waziri Shamuhuna alisema kwamba kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao
watakuwa na wasiwasi wa kutowaona ndugu na jamaa zao amewataka kufika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa zaidi au kuripoti habari za kupotelewa kwa
ndugu au jamaa zao.
Kwa upande wa Zanzibar, Waziri huyo aliwataka wananchi kufika kwa Masheha wao kutoa
taarifa kama hizo.
Serikali imewashukuru makampuni binafsi za usafiri baharini kwa msaada wao na wasisite kutoa
msaada katika kazi inayoendelea ya kutafuta watu au maiti wengine katika eneo la tukio.
Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe umbali wa maili sita
kuelekea Kusini mwa Kisiwa kidogo cha Yasin Zanzibar ikitokea Bandari ya Dar es Salaam
ilikoanza safari saa 5:30 asubuhi.
Meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Sea Guall Sea Transport Ltd, Kampuni ambayo Meli yake
nyengine ya Mv. Fatih ilizama ikiwa Bandarini Malindi Zanzibar na kufariki watu sita mwaka
2009.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
ZANZIBAR, TANZANIA
JULAI 19,2012
Mjumbe; " Mwenyekiti, Umekuwa Kimya Sana Hadi.....!"
Mr.Chairman-Bado uko ukweni??Umekuwa kimya sana hadi blog inaanza kudorora. David V
Jibu:
Asante sana David,
Ni
kweli, nimekuwa kimya. Huku nilipo mawasiliano pia ya tabu. Ni ya
kuvizia tu. Lakini natumia muda huu kufanya niyapendao, ikiwemo hili la
kuvua samaki. Unapovua samaki unatulia, unakaa kimya, unatafakari kwa
kina pia.
Hata hivyo nitajitahidi kuwarushia yale niwezayo kuyarusha.
Maggid,
Sweden
Ni Zaidi Ya Kitonga...!
Tawi la Chadema Washington DC limepokea Mwanachama Mpya Ambae Pia Amezawadia Tawi Hilo Zawadi Ya Gari Ili Kufanikisha Shuhuli Za Chama Hicho
Mwenyeketi
wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe.
Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe
wakimkabidhi rasmi Hussein Kauzel Msabaha kadi ya uwanachama.
Hussein Kauzel Msabaha akiwa na kadi ya Chadema
Daftari la Sera ya Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Hussein
Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama
Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi
Wanachama wa tawi la chadema Washington DC wakipata picha ya pamoja
Hussein
Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama
Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi.
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi akionyesha funguo za gari ya aina ya Chevy Suburban walilokabidhiwa na Hussein Kauzel Msabaha
Gari ya aina ya Chevy Suburban walilozawadiwa Chadema na Hussein Kauzel Msabaha
Siku
ya Jumamosi Juni 23, 2012, Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA
Washington DC lapokea zawadi ya gari aina ya Chevy Suburban kutoka kwa
Hussein Kauzel Msabaha, baada ya kukabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama
mpya wa chama hicho jijini Washington DC
kiongea
katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley
Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo
litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi
Majimbo mengine ya Marekani.
Naye
mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa
kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana
na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa
kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa
Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze
kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu
kwenye kukijenga Chama.
Picha na Habari na Mdau SwahiliVilla
Picha na Habari na Mdau SwahiliVilla
Chanzo: Haki Ngowi; http://www.blogger.com